Posts

Showing posts from March, 2018

ZLATAN APUNGUZA MSHAHARA 95% LA GALAXY

Image
https://ift.tt/2IkeENf MARA baada ya Zlatan Ibrahimovic kutangaza kusajiliwa na LA Galaxy ya Marekani, wengi wakawa wanajiuliza juu ya malipo ambayo atakuwa akilipwa, lakini imebainika kuwa ni pungufu ya yale aliyokuwa akilipwa alipokuwa Manchester United. Zlatan alikuwa akilipwa euro 21.8m (Sh bilioni 60.5) kwa mwaka lakini sasa atalipwa euro 1.2m (Sh bilioni 3) ikiwa ni pungufu ya asilimia 95 ya kiwango cha mshahara aliokuwa akilipwa, hiyo inamaanisha kuwa atakuwa akilipwa pauni 16,000 (Sh milioni 44) kwa wiki. Kutokana na kanuni za Marekani kuweka kiwango maalum kwa malipo ya mchezaji imelazimika Zlatan akubali kupokea mshahara mdogo lakini utakuwa na posho nyingi.

SERENA WILLIAM; TUZO NA MAFANIKIO YAKE HAVIKUTOKEA KAMA AJALI

Image
https://ift.tt/2J9ffT6 NI mcheza tenesi wa kimataifa kutoka Marekani, anashika namba moja duniani kwa upande wa wanawake na anatajwa kuwa mcheza tenesi bora wa muda wote. Alianza kuwa mchezaji wa tenesi bora wa kwanza duniani Julai 8, 2002. Mwaka, 2015, alikuwa ni mwanamichezo wa pili wa kike kulipwa pesa ndefu duniani akikunja dola za Kimarekani milioni 24.6 ambazo ni zaidi ya bilioni 50 za Kitanzania. Kama haitoshi Julai 18, 2016 alitajwa kuwa mcheza tenesi bora namba moja duniani kwa wiki 179 mfululizo. Lakini pia amefanikiwa kuweka rekodi ya kuwa mcheza tenesi wa kike pekee kuchukua tuzo 10 za Grand Slam katika miongo miwili tofauti. Hata hivyo, tuzo yake ya 38, katika tuzo mbalimbali alizowahi kuvuna ilimfanikisha kuwa namba nne katika listi ya wacheza tenesi wa muda wote, lakini namba mbili kwa wacheza tenesi ambao bado wanashiriki kwenye mchezo huo. Ni nani huyu? Si mwingine bali ni Serena Williams, mdogo wa damu wa mcheza tenesi bora duniani, Venus Williams na mama wa mtoto...

ANGALIA ANTHONY JOSHUA NA JOSE PARKER WALIVYOKINUKISHA WAKIPIMA UZITO

Image
https://ift.tt/2E6mKGE Mara baada ya zoezi hilo la vipimo kukamilika wawili hao Anthony Joshua na Joseph Parker kila mmoja amepata kuzungumza na vyombo vya habari na ndipo tambo zikaanza. Wakati mabondia hao walipokutana hii leo kwenye zoezi la kupima uzito Cardiff Najiskia vema, mazoezi yangu yamekwenda vizuri nadhani umeona mwenyewe nimepungua hadi kilo. Kupungua kwangu uzito kutaniongezea kuwa mwepesi na haraka zaidi kuliko hata mwanzo. Mpinzani wangu namuona yupo vizuri na nibingwa wa dunia ila nitafanya vizuri usiku wa kesho mwenye utashuhudia na nimejiskia furaha kuonana nae uso kwa uso kama hivi. Mimi ni bingwa wa dunia kwa hiyoa akilini mwangu najua naenda kukutana na bingwa mwenzangu wa WBO. Kwa upande wa Joseph Parker amesema kuwa yupo tayari kwa pambano hilo linalotarajiwa kupigwa hapo kesho siku ya Jumamosi.Mpaka hapa tulipofikia kilakitu kimekamilika wachanifikirie kuhusu pambano hili kwa kuwa najua atakuwa yupo makini.Tunafanana, sote tutakuwa na malengo sawa ulingon...

ANGALIA PICHA MAPOKEZI YA ZLATAN IBRAHIMOVIC ALIVYOTUA MAREKANI

Image
https://ift.tt/2J7jYVm Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic amepokelewa kifalme na mashabiki wa timu yake mpya ya LA Galaxy ya nchini Marekani. Ibrahimovic alitua katika uwanja wa ndege wa Los Angeles International Airport na kukutana na umati mkubwa wa mashabiki wa LA Galaxy. March 23 ya mwaka huu, Zlatan alisaini mkataba wa kujiunga na timu hiyo ambayo inashiriki ligi kuu ya Marekani.

Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 30.03.2018: Isco ameendelea kutafutwa, Robert Lewandowski naye anaitaka Madrid

https://ift.tt/eA8V8J Manchester City wanaamini wanaweza kusaini makataba na mchezaji wa kiungo cha kati wa Real Madrid mHispania Isco msimu huu wa majira ya joto

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 29.03.2018: Manchester City kuzungumza na Sterling, Chelsea wanamtaka kinda wa miaka 15

https://ift.tt/eA8V8J Timu mbali mbali za soka barani Ulaya zinahaha kujipanga kwa kuwasaka wachezaji bora wa kujiunga na timu zao wakati wa msimu ujao wa majira ya joto

Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 28.03.2018: Gabriel Jesus amekataa mshahara mpya, City wanamtaka Isco

https://ift.tt/eA8V8J Mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus, mwenye umri wa miaka 20, amekataa malipo ya £90,000- kutoka kwa viongozi wa Ligi ya Primia

BRAZIL WAITANDIKA UJERUMANI BAO 0-1, MECHI ZA KIRAFIKI KUELEKEA KOMBE LA DUNIA

Image
https://ift.tt/2IVp4DX Gabriel Jesus akishangilia baada ya kufunga bao. Wachezaji wa Brazil wakishangilia kwa pamoja. TIMU ya Brazil usiku wa kuamkia leo wameshinda dhidi ya wenyeji wake Ujerumani waliokuwa nyumbani katika mechi ya kirafiki ya Kalenda ya Fifa bao 1-0. Gabriel Jesus ndiye aliyefunga bao hilo. Inakuwa ni furaha kubwa kwa Brazil ambayo iliingia uwanjani na kumbukumbu ya kipigo cha mwisho cha mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani mara ya mwisho katika Kombe la Dunia. Germany (4-2-3-1): Trapp; Kimmich; Boateng (Sule 67); Rudiger; Plattenhardt; Gundogan (Werner 80); Kroos; Goretzka (Brandt 61); Draxler; Sane (Stindl 61); Gomez (Wagner 62) Brazil (4-3-3): Alisson; Alves; Silva; Miranda; Marcelo; Fernandinho; Casemiro; Paulinho; Willian; Jesus; Coutinho (Costa 72) Scorers: Jesus 37 MATOKEO MENGINE USIKU WA KUAMKIA LEO Russia 1-3 France Hungary 0-1 Scotland Denmark 0-0 Chile Poland 3-2 South Korea Belgium 4-0 Saudi Arabia Tunisia 1-0 Costa Rica Switzerland 6-0 Panama Ge...

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image
https://ift.tt/2GiqJ4G        

TAIFA STARS YAIBINYA KONGO 2-0 UWANJA WA TAIFA MECHI YA KIMATAIFA YA KIRAFIKI

Image
https://ift.tt/2ulwDAw Timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kupata ushindi wa magoli mawili dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa kwenye uwanja Taifa Jijini Dar es salaam. Kipindi cha pili timu zote zilikwenda bila ya kufungana kutokana na kushambuliana kwa zamu huku DRC walionesha kuliandama lango la Tanzania kwani vijana wa Mayanga walikuwa wakicheza kwa kujilinda Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko Ibrahim Ajib na Mudathiri Yahya walipoingia walibadilisha Mchezo na kuanza kushambulia kwa nguvu dakika ya 74 Mbwana Samatta aliwainua mashabiki wa soka kwa kufunga bao tamu kwa kichwa akimalizia krosi ya Kichuya kutoka upande wa kulia baada ya kazi nzuri ya Simon Msuva. Kichuya akaifungia Tanzania bao la pili dakika ya 88 akimalizia pasi ya Samatta baada ya kazi nzuri ya winga wa Difaa Hassan El Jadidi ya Morocco, Simon Msuva. Tanzania iliingia kwenye mchezo wa leo ikitoka kufungwa 4-...

MAJIBU YA DAKTARI SIMBA BAADA YA MKUDE KUUMIA JANA

Image
https://ift.tt/2pEWwqr Kiungo wa klabu ya Simba, Jonas Mkude amepata majeraha ya kifundo cha mguu wa kulia (Ankle) wakati akiwa kwenye mazoezima timu hiyo hapo jana. Daktari wa kikosi hicho cha Simba, Yassin Gembe amesema kuwa Mkude ameumia kwenye kifundo cha mguu wa kulia na haonekani kuwa amepata majeraha makubwa. Mkude ameumia kwenye kifundo cha mguu wa kulia, kwa vipimo vya awali sio majeraha makubwa sana, ila kesho ndio tutatoa taarifa kamili kuhusianana na hali yake kwa ujumla ila kwa sasa napenda kusema anaendelea vizuri kutoka katika matibabu ya awali tuliyompatia” amesema Gembe. Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara amesema kuwa kiungo huyo anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda wa siku mbili hadi tatu.

BREAKING: SIMBA VS YANGA HATIMAYE KIMEELEWEKA

Image
https://ift.tt/2pJMCCX Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kupitia Mtendaji Mkuu, Boniface Wambura leo imetangaza rasmi tarehe ambayo Watani wa Jadi (Simba SC na Yanga SC) watakutana kucheza mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Wambura amesema timu hizo sasa zitacheza tarehe 29 Aprili 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi ambayo Simba atakuwa mwenyeji wa pambano hilo. Awali Bodi ya Ligi ilikuwa haijaweka tarehe hiyo wazi kutokana na mambo mbalimbali kuingiliana na kufanya ratiba ya mchezo huo kutopangwa kwa wakati. Timu hizi zenye wafuasi wengi nchini, zilikutana Oktoba 28 2017 kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi na kwenda sare ya bao 1-1, huku wafungaji wa mabao hayo wakiwa ni Shiza Kichuya upande wa Simba na Obrey Chirwa kwa Yanga. Pamoja na michezo mingine mbalimbali ambayo leo imetolewa ratiba yake rasmi, klabu ya Simba imepangwa kucheza; Njombe Mji FC Vs Simba April 3 Mtibwa vs Simba Aprili 9 Lipuli FC vs Simba Aprili 20 Simba vs Yanga Aprili 29.

Roman Torres: Shujaa wa Panama anayepanga kuwahangaisha England Kombe la Dunia Urusi

https://ift.tt/eA8V8J Roman Torres ana umaarufu sawa na wa nyota wa filamu nchini mwake baada ya kufunga bao lililowawezesha Panama kufuzu kwa kOmbe la Dunia, na anasema hamuogopi Harry Kane.

Jose Mourinho alalama hakuna anayeishabikia Man United

https://ift.tt/eA8V8J Jose Mourinho alalama hakuna anayeishabikia Man United

Tetesi za soka Ulaya Jumapili 25.03.2018

https://ift.tt/eA8V8J Manchester United iko tayari kumuuza kiungo wa Ufaransa ,25 Paul Pogba

Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 24.03.2018

https://ift.tt/eA8V8J Manchester City na Manchester United zote kwa pamoja zitapambana kujaribu kumsajili nyota wa Brazil Neymar iwapo ataamua kuondoka Paris St-Germain

UREDO WAITANDIKA MISRI,RONALDO AMFANYIA SALAH KITU MBAYA

Image
https://ift.tt/2G113Of MWANASOKA bora wa dunia anayeichezea Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kuonesha ubabe wake mbele ya nyota wa Misri, anayefanya vizuri kwasasa na klabu yake ya Liverpool, Mohamed Salah baada ya kuisawadhishia Ureno na kufunga bao la ushindi katika mechi baina ya timu hizo za taifa. Ronaldo ameonesha umwamba huo kwenye mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA ambapo timu yake ya Ureno ilikuwa mwenyeji wa Misri na ilikubali kuwa nyuma kwa bao la Salah hadi dakika ya 90 kabla ya Ronaldo kubadili mambo. Salah aliitanguliza Misri kwa bao la dakika ya 56 kisha Ronaldo kuamua ushindi wa mabao 2-1 kwa timu yake ya Ureno kwa mabao ya dakika ya 90+2 na 90+4. Baada ya mabao hayo mawili Ronaldo sasa amefikisha jumla ya mabao 81 ya kuifungia timu yake ya taifa akiwa ndio mchezaji mwenye mabao mengi zaidi akifuatiwa na Messi mwenye mabao 61 aliyoifungia Argentina. Mohamed Salah kwasasa ndio anaongoza mbio za ufungaji bora kwenye ligi...

ANGALIA ZLATAN IBRAHIMOVIC ALIVYOTUA LA GALAXY

Image
https://ift.tt/2FZTMhr Staa wa Sweden aliyekuwa anaichezea Man United ya England Zlatan Ibrahimovicametumia style ya kipekee kuutangazia umma kuwa kwa sasa anaenda kucheza soka Marekani katika club ya LA Galaxy inayoshiriki Ligi Kuu Marekani MLS. Unaambiwa Zlatan amelipia ukurasa mzima wa gazeti la LA Times na kuandika tangazo maalum kuhusu ujio wake mpya katika club hiyo, ukurasa huo umeandika stori kuhusu ujio wa Zlatan na kutoa picha ya Zlatan akiwa amevaa jezi za LA Galaxy. Taarifa hiyo iliyotolewa na gazeti la LA Times Sport imeandika kuwa kwa sasa Zlatan Ibrahimovic anawasili katika club hiyo likiwa ni jina kubwa zaidi ya David Beckhamaliyejiunga timu hiyo miaka kadhaa iliyopita, Zlatan anaondoka Man United baada ya kuitumikia katika game 53, kafunga magoli 29 akitoa assist 10.

MAN UTD NA ZLATAN IBRAHIMOVIC WAMALIZANA,KUONDOKA RASMI

Image
http://ift.tt/2pu7FdG Masaa machache yaliyopita mtandao wa metro.co.uk umeripoti kuwa maisha ya staa wa soka wa kimataifa wa Sweden anayeichezea Man United ya England Zlatan Ibrahimovic maisha yake ndani ya Man United yameisha na ataihama club hiyo na kuelekea nchini Marekani kucheza Ligi Kuu ya nchi hiyo MLS. Zlatan ambaye alijiunga na Man United 2016 kama mchezaji huru akitokea Paris Saint Germain ya Ufaransa, katika kipindi hicho akiwa Man United amefanikiwa kuifungia Man United magoli 29 katika game 53 wastani wa goli moja kwa mechi mbili, huku akitoa assist 9 na ameshinda mataji matatu. Jeraha la goti la Zlatan limefanya aichezee Man United katika game saba pekee msimu huu na hajaichezea Man United toka Boxing Day katika game dhidi ya Burnley iliyomalizika kwa Man United kupata sare ya kufungana magoli 2-2, taarifa rasmi inatajwa kuwa itatolewa siku zijazo lakini za chini ya kapeni zinaeleza kuwa Mourinho amempa baraka Zlatan ya kujiunga na LA Galaxy.

ANGALIA MESI APEWA MBINU ZA KUSHINDA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2018

Image
http://ift.tt/2pyf1vR Mwanamke anayetajwa kuwa na ushawishi mkubwa duniani, Oprah Winfrey ametoa ushauri kwa mshambuliaji wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi jinsi ya kushinda Kombe la Dunia la mwaka huu. Lionel Messi na Oprah Winfrey Akiwa kwenye mahojiano na kituo cha Proto TV cha nchini Argentina, Oprah amesema kuwa anaamini huu ni wakati sahihi wa Messi kuchukua kombe hilo lenye heshima kubwa duniani lakini ni lazima aongeze nguvu uwanjani. Oprah (64) amesema kuwa Messi anatakiwa acheze kwa kuingia katikati kwenye uwanja na aongeze nguvu ya kuamini kwenye nafsi yake kama anataka kushinda kombe la dunia. “Messi ujumbe huu ni maalumu kwako na najua utaupata, unatakiwa ucheze kwa nguvu zako zote ukiwa uwanjani, na uwe na nguvu ya imani kwenye nafsi yako pindi unapokuwa uwanjani, nadhani Messi utakuwa shujaa,“amesema Oprah baada ya kuombwa na mtangazaji wa kituo hicho kutoa ushauri kwa Messi kuelekea kombe la dunia. Kwenye mahojiano hayo Oprah aliongozan...

SIMBA SC YAONDOA WATANO KIKOSI KITACHOIVAA YANGA SC

Image
http://ift.tt/2u6U1lv KUELEKEA mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga ambao awali ulipangwa kuchezwa Aprili 7, mwaka huu, tayari baadhi ya wachezaji wa timu hizo hawataweza kucheza mchezo huo kama walivyofanya kule nyuma. Katika msimamo wa ligi hiyo, timu hizo kwa sasa zinatofautiana mabao ya ku­funga lakini zikiwa sawa pointi kwa pointi 46, Simba ipo kileleni ikifuatiwa na Yanga ingawa Simba wana mchezo mmoja mkononi. Mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Oktoba 28, mwaka jana ambao ulimal­izika kwa sare ya bao 1-1, vikosi vilivyoanza vya timu hizo mbili ni tofauti na vile ambavyo vinatarajiwa kuku­tana mwezi ujao. Kuelekea mchezo huo, kwa upande wa Simba wache­zaji ambao watakuwa wapya ambao kwa sasa wamekuwa wakicheza kikosi cha kwanza ni Asante Kwasi, Nicholaus Gyan, Shomari Kapombe, Jonas Mkude na John Bocco ambao wote hawakucheza mchezo wa kwanza. Ambao wameondolewa kwenye kikosi ni Mohamed Ibrahim ‘Mo’, Method Mwanjale, Haruna Niy­onzima, Mzamiru Yassin na Laudit Mavu...

Veronica Mbithe: Bondia wa Kenya aamua heri jeshi kuliko Michezo ya Jumuiya ya Madola

http://ift.tt/eA8V8J Bondia wa Kenya Veronica Mbithe amejiondoa kwa timu ya taifa ya ndondi itakayoshiriki michezo ya Jumuiya ya Madola mwezi ujao mjini Gold Coast, Australia.

Heather Watson atupwa nje michuano ya Miami

http://ift.tt/eA8V8J Mchezaji wa tenisi Heather Watson ametupwa nje ya michuano ya wazi ya Miami katika mchezo wa kwanza dhidi ya mbrazili Beatriz Haddad Maia

Jose Mourinho: Mkufunzi wa Manchester United anaonekana kupitwa na wakati - Chris Sutton

http://ift.tt/eA8V8J Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anaonekana kupitwa na wakati na tabia zake zimebadilika , kulingana na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Chris Sutton.

Cristiano Ronaldo afunga hat-trick yake ya 50

http://ift.tt/eA8V8J Cristiano Ronaldo alifunga hat-trick yake ya 50 tangu aanze kucheza soka ya kulipwa huku Real Madrid ikiilaza Girona na hivyobasi kupanda hadi nafasi ya tatu katika ligi ya La Liga.

REAL MADRID YAICHAPA GIRONA 6-3, RONALDO ATUPIA NNE

Image
http://ift.tt/2FR9VBD KLABU ya Real Madrid wakiwa nyumbani imeinyuka vilivyo timu ya Girona kwa bao 6-3 katika mechi ya Ligi Kuu Hispania ‘La Liga Santanda’ jana Jumapili, Machi 18, 2018 katika uwanja wa Santiago Bernabeu. Katika mechi hiyo iliyokuwa na mvuto wa aina yake huku Ronaldo akiandika rekodui nyingine baada ya kugonga hat trick ya 50 katika maisha yake ya soka baada ya kutupia mabao 4 kambani peke yake. Ronaldo aliweka wavuni mabao yake kunako dakika ya 11, 47, 64 na ya 90+1, huku Lucas Vazquez akiifungia Madrid bao la 5 dakika ya 59 na Bale dakika ya 86. Kwa upande wa Girona mabao yao yalifungwa na Stuani dakika ya 29 na 67 na Juanpe dakika ya 88 mchezo huo. Kwa mabao hayo, Ronaldo afikisha mabao 22 ya Laliga mbele ya Suarez mwenye mabao 21 huku Messi akiongoza kwa kuwa na mabao 25. Kwa matokeo hayo, Madri wanabaki nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 60 nyuma ya Atletico Madrid wenye pointi 64 na vinara barcelona wakiongoza kwa pointi 75. Real Ma...