ANGALIA ANTHONY JOSHUA NA JOSE PARKER WALIVYOKINUKISHA WAKIPIMA UZITO

https://ift.tt/2E6mKGE

Mara baada ya zoezi hilo la vipimo kukamilika wawili hao Anthony Joshua na Joseph Parker kila mmoja amepata kuzungumza na vyombo vya habari na ndipo tambo zikaanza.
Wakati mabondia hao walipokutana hii leo kwenye zoezi la kupima uzito Cardiff
Najiskia vema, mazoezi yangu yamekwenda vizuri nadhani umeona mwenyewe nimepungua hadi kilo. Kupungua kwangu uzito kutaniongezea kuwa mwepesi na haraka zaidi kuliko hata mwanzo.
Mpinzani wangu namuona yupo vizuri na nibingwa wa dunia ila nitafanya vizuri usiku wa kesho mwenye utashuhudia na nimejiskia furaha kuonana nae uso kwa uso kama hivi. Mimi ni bingwa wa dunia kwa hiyoa akilini mwangu najua naenda kukutana na bingwa mwenzangu wa WBO.

Kwa upande wa Joseph Parker amesema kuwa yupo tayari kwa pambano hilo linalotarajiwa kupigwa hapo kesho siku ya Jumamosi.Mpaka hapa tulipofikia kilakitu kimekamilika wachanifikirie kuhusu pambano hili kwa kuwa najua atakuwa yupo makini.Tunafanana, sote tutakuwa na malengo sawa ulingoni hapo kesho nimemuona ni mtu mwenye kujiamini ninaamini ni mpambanaji mzuri.
Parker ameongeza Raundi za mwanzo chochote kinaweza kutokea itategemea kila mmoja ameingia na mpango upi mzuri zaidi ya mwenzake, nipo tayari kwa chochote. Nipo hapa kwa vita utalazimika kufanya kilakitu ili uweze kunipiga.
AJ mwenye umri wa miaka 28 ataingia uwanja wa Principality uliyopo Cardiff huku akiwa na rekodi ya kutopoteza pambano hata moja kati ya 20 yote aliyocheza na kumkabili mpanzani wake Parker ambaye na haja poteza hata moja kati ya 24 aliyopigana.
Wawili hao wataingia uwanjani hapo kesho siku ya Jumamosi ya tarehe 31 ya mwezi Machi kila mmoja kutaka kutengeneza historia yake.

Popular posts from this blog