BREAKING: SIMBA VS YANGA HATIMAYE KIMEELEWEKA
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kupitia Mtendaji Mkuu, Boniface Wambura leo imetangaza rasmi tarehe ambayo Watani wa Jadi (Simba SC na Yanga SC) watakutana kucheza mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Wambura amesema timu hizo sasa zitacheza tarehe 29 Aprili 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi ambayo Simba atakuwa mwenyeji wa pambano hilo.
Awali Bodi ya Ligi ilikuwa haijaweka tarehe hiyo wazi kutokana na mambo mbalimbali kuingiliana na kufanya ratiba ya mchezo huo kutopangwa kwa wakati.
Timu hizi zenye wafuasi wengi nchini, zilikutana Oktoba 28 2017 kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi na kwenda sare ya bao 1-1, huku wafungaji wa mabao hayo wakiwa ni Shiza Kichuya upande wa Simba na Obrey Chirwa kwa Yanga.
Pamoja na michezo mingine mbalimbali ambayo leo imetolewa ratiba yake rasmi, klabu ya Simba imepangwa kucheza;
Njombe Mji FC Vs Simba April 3
Mtibwa vs Simba Aprili 9
Lipuli FC vs Simba Aprili 20
Simba vs Yanga Aprili 29.