MAJIBU YA DAKTARI SIMBA BAADA YA MKUDE KUUMIA JANA

https://ift.tt/2pEWwqr

Kiungo wa klabu ya Simba, Jonas Mkude amepata majeraha ya kifundo cha mguu wa kulia (Ankle) wakati akiwa kwenye mazoezima timu hiyo hapo jana. Daktari wa kikosi hicho cha Simba, Yassin Gembe amesema kuwa Mkude ameumia kwenye kifundo cha mguu wa kulia na haonekani kuwa amepata majeraha makubwa.

Mkude ameumia kwenye kifundo cha mguu wa kulia, kwa vipimo vya awali sio majeraha makubwa sana, ila kesho ndio tutatoa taarifa kamili kuhusianana na hali yake kwa ujumla ila kwa sasa napenda kusema anaendelea vizuri kutoka katika matibabu ya awali tuliyompatia” amesema Gembe.

Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara amesema kuwa kiungo huyo anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda wa siku mbili hadi tatu.

Popular posts from this blog