ANGALIA MESI APEWA MBINU ZA KUSHINDA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2018

http://ift.tt/2pyf1vR

Mwanamke anayetajwa kuwa na ushawishi mkubwa duniani, Oprah Winfrey ametoa ushauri kwa mshambuliaji wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi jinsi ya kushinda Kombe la Dunia la mwaka huu. Lionel Messi na Oprah Winfrey Akiwa kwenye mahojiano na kituo cha Proto TV cha nchini Argentina, Oprah amesema kuwa anaamini huu ni wakati sahihi wa Messi kuchukua kombe hilo lenye heshima kubwa duniani lakini ni lazima aongeze nguvu uwanjani.

Oprah (64) amesema kuwa Messi anatakiwa acheze kwa kuingia katikati kwenye uwanja na aongeze nguvu ya kuamini kwenye nafsi yake kama anataka kushinda kombe la dunia. “Messi ujumbe huu ni maalumu kwako na najua utaupata, unatakiwa ucheze kwa nguvu zako zote ukiwa uwanjani, na uwe na nguvu ya imani kwenye nafsi yako pindi unapokuwa uwanjani, nadhani Messi utakuwa shujaa,“amesema Oprah baada ya kuombwa na mtangazaji wa kituo hicho kutoa ushauri kwa Messi kuelekea kombe la dunia.

Kwenye mahojiano hayo Oprah aliongozana pia na Muigizaji wa filamu Reese Witherspoon naye amesema kuwa itakuwa mwaka huu Messi atafikisha miaka 30 na ni muda wake kuchukua kombe la dunia. Oprah anatajwa kuwa ni miongoni mwa watu wenye ushawishi mkubwa duniani na kauli zake huwa zinaaminika sana na watu wa rika zote.

Messi anayetajwa kuwa ni mchezaji bora wa muda wote ameshinda makombe makubwa karibia yote akiwa na klabu ya Barcelona lakini hajawahi kushinda kombe la dunia akiwa na timu yake ya taifa ya Argentina.

Popular posts from this blog