SIMBA SC YAONDOA WATANO KIKOSI KITACHOIVAA YANGA SC

http://ift.tt/2u6U1lv

KUELEKEA mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga ambao awali ulipangwa kuchezwa Aprili 7, mwaka huu, tayari baadhi ya wachezaji wa timu hizo hawataweza kucheza mchezo huo kama walivyofanya kule nyuma. Katika msimamo wa ligi hiyo, timu hizo kwa sasa zinatofautiana mabao ya ku­funga lakini zikiwa sawa pointi kwa pointi 46, Simba ipo kileleni ikifuatiwa na Yanga ingawa Simba wana mchezo mmoja mkononi.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Oktoba 28, mwaka jana ambao ulimal­izika kwa sare ya bao 1-1, vikosi vilivyoanza vya timu hizo mbili ni tofauti na vile ambavyo vinatarajiwa kuku­tana mwezi ujao. Kuelekea mchezo huo, kwa upande wa Simba wache­zaji ambao watakuwa wapya ambao kwa sasa wamekuwa wakicheza kikosi cha kwanza ni Asante Kwasi, Nicholaus Gyan, Shomari Kapombe, Jonas Mkude na John Bocco ambao wote hawakucheza mchezo wa kwanza.

Ambao wameondolewa kwenye kikosi ni Mohamed Ibrahim ‘Mo’, Method Mwanjale, Haruna Niy­onzima, Mzamiru Yassin na Laudit Mavugo, ukiachana na Mwanjale ambaye ameachwa, wengine ni wag­onjwa na wengine hawana nafasi kikosi cha kwanza. Yanga wenyewe licha ya kusuasua msimu huu kuto­kana na kuandamwa na ma­jeruhi wengi kikosi chao cha mchezo ujao kinaweza kisiwe na mabadiliko makubwa kama ilivyokuwa kwa upande wa Simba.

Wachezaji ambao ni wapya kwa upande wa Yanga atakuwa ni Hassan Kessy, Said Juma Makapu na Em­manuel Martin ambao ndiyo wameweza kuingia kwenye kikosi cha kwanza kwa muda mrefu tangu umalizike mch­ezo huo wa watani wa jadi. Wale ambao waliku­wepo kwenye kikosi cha kwanza wakati timu hizo zilipopambana awali, Juma Abdul, Geoffrey Mwashiuya na Raphael Daudi, wam­eonekana kupoteza nafasi zao kwa sasa kwenye kikosi cha kwanza. STORI: MARTHA MBOMA | GLOBAL PUBLISHERS

Popular posts from this blog