REAL MADRID YAICHAPA GIRONA 6-3, RONALDO ATUPIA NNE

http://ift.tt/2FR9VBD

KLABU ya Real Madrid wakiwa nyumbani imeinyuka vilivyo timu ya Girona kwa bao 6-3 katika mechi ya Ligi Kuu Hispania ‘La Liga Santanda’ jana Jumapili, Machi 18, 2018 katika uwanja wa Santiago Bernabeu.
Katika mechi hiyo iliyokuwa na mvuto wa aina yake huku Ronaldo akiandika rekodui nyingine baada ya kugonga hat trick ya 50 katika maisha yake ya soka baada ya kutupia mabao 4 kambani peke yake.
Ronaldo aliweka wavuni mabao yake kunako dakika ya 11, 47, 64 na ya 90+1, huku Lucas Vazquez akiifungia Madrid bao la 5 dakika ya 59 na Bale dakika ya 86.
Kwa upande wa Girona mabao yao yalifungwa na Stuani dakika ya 29 na 67 na Juanpe dakika ya 88 mchezo huo.
Kwa mabao hayo, Ronaldo afikisha mabao 22 ya Laliga mbele ya Suarez mwenye mabao 21 huku Messi akiongoza kwa kuwa na mabao 25.

Kwa matokeo hayo, Madri wanabaki nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 60 nyuma ya Atletico Madrid wenye pointi 64 na vinara barcelona wakiongoza kwa pointi 75.


Real Madrid (4-4-2): Navas; Carvajal, Varane, Nacho, Marcelo; Lucas Vazquez, Kovacic (Modric 70), Kroos, Asensio (Bale 70); Benzema (Isco 83), Ronaldo

Unused subs: Casilla, Theo H., Vallejo, Casemiro

Goals: Ronaldo 11, 47, 64, 90+1, Lucas Vazquez 59, Bale 86

Bookings: Carvajal 52, Granell 90+3

Girona (3-4-2-1): Bono; Ramalho, Bernardo, Juanpe; Maffeo (Aday 83), Pere Pons, Granell, Mojica; Portu, Borja Garcia (Lozano 69), Stuani (Olunga 87)

Unused subs: Iraizoz, Muniesa, Copovi, Aleix Garcia

Goals: Stuani 29, 67, Juanpe 88

Booking: Mojica 30.

Popular posts from this blog