MAN UTD NA ZLATAN IBRAHIMOVIC WAMALIZANA,KUONDOKA RASMI

http://ift.tt/2pu7FdG

Masaa machache yaliyopita mtandao wa metro.co.uk umeripoti kuwa maisha ya staa wa soka wa kimataifa wa Sweden anayeichezea Man United ya England Zlatan Ibrahimovic maisha yake ndani ya Man United yameisha na ataihama club hiyo na kuelekea nchini Marekani kucheza Ligi Kuu ya nchi hiyo MLS.

Zlatan ambaye alijiunga na Man United 2016 kama mchezaji huru akitokea Paris Saint Germain ya Ufaransa, katika kipindi hicho akiwa Man United amefanikiwa kuifungia Man United magoli 29 katika game 53 wastani wa goli moja kwa mechi mbili, huku akitoa assist 9 na ameshinda mataji matatu.

Jeraha la goti la Zlatan limefanya aichezee Man United katika game saba pekee msimu huu na hajaichezea Man United toka Boxing Day katika game dhidi ya Burnley iliyomalizika kwa Man United kupata sare ya kufungana magoli 2-2, taarifa rasmi inatajwa kuwa itatolewa siku zijazo lakini za chini ya kapeni zinaeleza kuwa Mourinho amempa baraka Zlatan ya kujiunga na LA Galaxy.

Popular posts from this blog