http://ift.tt/2DwdlZh Kikosi cha Yanga kimetua salama Mjini Mwanza tayari kwa pambano lake la Jumapili dhidi ya wenyeji Mbao FC, pambano la Ligi Kuu ambalo limepangwa kupigwa uwanja wa CCM Kirumba. Kocha msaidizi wa timu hiyo Shadrack Nsajigwa amesema, timu imewasili salama na leo wanatarajia kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Kirumba, pamoja na kesho kabla ya kujiandaa na mchezo huo ambao wameupa umuhimu mkubwa. Nashukuru tumewasili salama Mwanza, hali ya hewa ni nzuri na kufika mapema siku mbili kabla ya mchezo kutatusaidia kufanya vizuri kwenye mchezo wetu wa keshokutwa kwasababu tumedhamiria kushinda mchezo huo ukizingatia Mbao ni timu nzuri na imeuwa ikitusumbua sana,” amesema Nsajigwa. Kocha huyo amesema ukitoa wachezaji Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa wachezaji wote waliobaki na kusafiri na timu hiyo niwazima na wapo katika ari kubwa ya kuhakikisha wanacheza na kuhakikisha wanapata pointi tatu. Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ikiw...