WEMA AMTUMIA SALAMU NZITO HAJI MANARA KISA HIKI HAPA
Msanii Wema Sepetu, ametuma salamu kwa mkuu wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Manara, na kutamba kwa kusema, klabu ya Yanga ndio timu kubwa na yenye mafanikio hapa nchini na kitendo cha kufungwa na Simba katika mchezo wa April 29 ni sehemu ya mchezo tu.
Akiongea na waandishi wa habari Mei 02 wakati wa kutambulishwa kama balozi wa Startimes kueleka kombe la dunia, Wema amesema yeye ni mpenzi mkubwa wa timu Yanga na hata katika kuchukua ubingwa timu hiyo imefanikiwa zaidi kuliko wapizani wao simba.
“Mpelekeeni salamu Haji Manara, anajua kabisa kwamba Yanga tumechukua ligi (kuu bara) mara nyingi sana, kwa hiyo wao (Simba) kutufunga juzi ni changamoto, katika ubingwa huwa tunawachapa kilasiku”, amesema Wema
Haji Manara na msanii Wema Sepetu wamekua na tambo za maneno kuhusu timu za Simba Yanga hususani katika mitandao ya kijamii.
Akiongelea kuhusu nchi wakilishi wa bara la Afrika katika michuano ya kombe la dunia Wema amesema, bado kuna changamoto kubwa kwa nchi hizo kufanya vizuri katika michuano hiyo ukilinganisha na mataifa ya bara la Ulaya.