MANCHESTER UNITED WAIPA MAN CITY UBINGWA WA LIGI ENGLAND WATANDIKWA
https://ift.tt/2ELmIEl
Manchester United imefungwa 1-0 na West Brom, hatua ambayo inaipa rasmi Manchester City ubingwa wa Premier League. City ina jumla ya pointi 87 na ni Manchester United pekee ndiyo ingeweza kuzifikia iwapo ingeshinda mechi zake zote zilizosalia huku City ikitakiwa kupoteza zote.
United ikicheza kwenye dimba lake la Old Trafford, iliruhusu bao pekee la West Brom kunako dakika ya 73 kupitia kwa Jay Rodriguez.
Kwa matokeo hayo United yenye michezo 33 inabakiwa na pointi 71 na kama itashinda mechi zake tano zilizosalia itajikusanyia pointi 86.