MAN UTD WAITANDIKA MAN CITY NYUMBANI KWAO,POGBA AWASHA MOTO
KLABU ya Manchester United wakiwa ugenini wameitwanga timu ya Man City kwa jumla ya bao 3-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya uingereza ulimalizika usiku huu.
Man City walianza mchezo kwa kasi ya ajabu na kuwapoteza kabisa Man U, jambo ambalo liliwafanya kumiliki mpira kwa kiwango kikubwa katika kipindi chote cha kwanza.
Man City ambao ni vinara wa Ligi hiyo ndiyo walikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za United kunako dakika ya 25 kupitia kwa Vincent Kompany aliyemalizia mkwaju wa kona kwa kichwa chake.
Dakika 5 baadaye Ilkay Guendogan akaingia na kuiandikia Man City bao la pili ambalo lilidumu mpaka mwisho wa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Man U waliingia na moto wa kufa mtu huku wakiishambulia City kwa nguvu jitihada zilizozaa bao la kwanza kupitia kwa Paul Pogba kunako dakika ya 53.
Dakika mbili baadaye, Pogba alirudi tena nyavuni na kuandika bao la pili na la kusawadhisha kwa Man U kunako dakika ya 55 kabla ya Raheem Sterling kufunga bao la tatu na la kuongoza dakika ya 63.