ARSENAL YAITWANGA SOUTHAMPTON 3-2
KLABU ya Washika Bunduki wa Jiji la London, Arsenal ‘The Gunners’ wameipa dozi ya bao 3-2 klabu ya Southampton katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza ‘EPL’, mchezo uliopigwa jana.
Arsenal wakiwa nyumbani walianza kwa kuteteleka baada ya kuruhusu bao dakika za mapema kabisa za mchezo huo ambapo Shane Long aliifungia Southempton bao la kwanza dakika ya 17 tu ya mchezo huo.
hali ya mchezo ilibadilika kabisa na Arsenal kuanza kukomaaili warudishe bao hilo juhudi ambazo zilizaa matunda dakika 11 baadaye baaya Pierre-Emerick Aubameyang kuisawadhishia Arsenal kunako dakika ya 28.
Arsenal hawakukomea hapo, dakika 10 baadaye Danny Welbeck alichungulia nyavu za Southampton kunako dakika ya 38 na kuifanya Arsenal kuongoza kwa bao 2-1 hadi mapumziko.
Dakika ya 73, Charlie Austin akaisawadhishia Southampton hali iliyowatia kiwewe Arsenal na kuongeza mashambulizi zaidi ambapo dakika ya 81, Danny Welbeck aliiandikia Arsenal bao la 3 na kuongoza katika mchezo huo.
Katika game hiyo, Aubameyang tangu asajiliwe Arsenal dirisha dogo msimu huu amefikisha mechi saba alizocheza huku akifunga mabao 6 na assist 1.
Arsenal: (4-2-3-1): Cech 7.5; Bellerin 75 6 (Holding 6), Mustafi 4, Chambers 5.5, Kolasinac 6; Elneny 6, Xhaka 6.5; Nelson 5.5 (Wilshere 64), Iwobi 7.5, Welbeck 7.5; Aubameyang 8 (Lacazette 72 6)
Subs not used: Macey, Ozil, Monreal, Nketiah.
Manager: A Wenger 6
Southampton: (5-4-1): McCarthy 8; Soares 7.5, Stephens 5, Yoshida 5 (Austin 73), Hoedt 4.5, Bertrand 6.5; Ward-Prowse 5.5, Hojbjerg 6, Romeu 5.5, Tadic 7.5; Long 7 (Sims 79 6)
Subs not used: Forster, Boufal, Gabbiadini, Redmond, Pied
Manager: M. Hughes 7
Referee: A. Marriner (West Midlands) 5.