ANGALIA BONDIA ALIYEFARIKI DUNIA BAADA YA KUSHINDA PAMBANO
Mwanamasumbwi raia wa Uingereza, Scott Westgarth amefariki dunia akiwa hospitali baada ya kutwaa ubingwa wake dhidi ya Dec Spelman huko Doncaster. Westgarth mwenye umri wa miaka 31, alianguka katika chumba chake cha kubadilishia nguo siku ya Jumamosi kufuatia kutwaa mkanda kwa pointi raundi ya 10 dhidi ya Spelman.
Kwa upande wa promota wake, Stefy Bull kupitia mtandao wake wa Twitter amesema kuwa “Nimemshuhudia kijana akifanya kazi anayoipenda kiasi kwamba yupo tayari kuhatarisha hata maisha yake, sina maneno mengi ya kusema hasa katika kipindi hiki kigumu kwa familia, timu na marafiki hakika inauma,” amesema Bull. dec spelman @dec_spelman
Absolutely heartbroken and lost for words ail continue to pray for Scott’s family and the people close to him rest easy my friend xxx 11:58 AM – Feb 26, 2018 994 239 people are talking about this Twitter Ads info and privacy
Taarifa zinasema kuwa Westgarth ameonekana kuwa mwenye maumivu baada ya pambano hilo licha ya kuposti picha yake inayomuonyesha akisherehekea ushindi aliyo upata kabla ya kuanguka katika chumba cha kubadilishia nguo na kufikishwa hospitali ya Royal Hallamshire.