SIMBA WAITANDIKA MAJIMAJI BAO 4,OKWI NA BOKO WATUPIA MBILI

http://ift.tt/2DWBoEB

Simba ambayo imecheza mechi yake ya 15 kwenye ligi msimu bila kupoteza, mabao yake yamefungwa na washambuliaji Emmanuel Okwi na John Bocco, kila mmoja akifunga mabao mawili. 

Baada ya ushindi wa leo Simba sasa imefikisha alama 35 na kuendelea kuzikimbia timu za Azam FC yenye alama 30 kwenye nafasi ya pili na Yanga yenye alama 28 kwenye nafasi ya tatu.

Mechi nyingine ambayo imepigwa leo kuhitimisha mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ni Singida United ambayo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

Mzunguko wa pili wa ligi kuu unatarajiwa kuanza wikiendi ijayo lakini katikati ya wiki ijayo itachezwa michezo ya raundi ya tatu ya kombe la shirikisho.

Popular posts from this blog