MANCHESTER CITY WANASA BEKI GHALI DUNIANI
Klabu ya Manchester City kupitia tovuti yake imetangaza kumsajili beki wakati wa timu ya taifa ya Ufaransa, Aymeric Laporte.
Laporte mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na klabu ya Athletic Bilbao kabla ya meneja wa City,Pep Guardiola kumsajili kwa kwa dili litakalo muweka hapo mpaka mwaka 2023. Mlinzi huyo ambaye ni chaguo la Guardiola, atavaa jezi namba 14 na kuisaidia timu hiyo kushinda mataji mbali mbali.
Laporte mara baada ya kuingia kandarasi na City amesema “Ni mwenye furaha kubwa kuwa hapa katika timu yenye malengo makubwa na miongoni mwa klabu kubwa barani Ulaya,” amesema Laporte. Aymeric Laporte ameongeza
“Nitaendelea kupambana na kufanya kazi kwa juhudi nikiwa chini ya Pep Guardiola na kuisaidia timu kufikia mafanikio.” Laporte alianza soka la kulipwa akiwa na Bilbao mwaka 2012