KAULI YA HAJI MANARA BAADA YANGA KUSONGA MBELE KOMBE LA SHIRIKISHO

http://ift.tt/2ns4q4l

Jumanne ya January 30 2018 Yanga walikuwa katika uwanja wa Sokoine Mbeya kucheza mchezo wao wa round ya tatu wa Kombe la ASFC dhidi ya wenyeji wao Ihefu FC, katika mchezo huo Yanga waliojifunga mapema dakika ya 37 walilazimika kusubiri hadi dakika za nyongeza kabla ya game kuisha ndio wakasawazisha.

Dakika tatu za nyongeza kabla ya game kuisha Yanga walisawazisha kwa penati, hivyo dakika 90 zikamalizika kwa sare ya 1-1, mikwaju ya penati ilipopigwa Yanga akaibuka na ushindi wa penati 4-3, baada ya Yanga kusawazisha kwa penati afisa habari wa Simba Haji Manara aliandika ujumbe huu kwenye page yake ya instagram.

Hata Nyani hutamani pilau,mbeleko za baadhi ya maamuzi ni kichefuchefu..ndio maana baadhi ya team zikienda kwenye international competitions wanatutia aibu tu…Ndegelec!!” Haji Manara

Popular posts from this blog