Familia ya Sanchez pamoja na mbwa wake Atom na Humber wang’ara na jezi ya United
http://ift.tt/2n6vNAV
Katika kudhihirisha kuwa tayari ameshahamia Manchester United, mshambuliaji raia wa Chile, Alexis Sanchez ameamua kuivisha jezi ya timu hiyo familia yake na mbwa wake wawili ambao anawapenda Atom na Humber.
Alexis Sanchez akiwa amewavisha jezi ya Man United mbwa wake Atom na Humber Sanchez ametua rasmi Old Trafford siku ya Jumatatu katika dili ambalo linamfanya kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi katika ligi ya Uingereza.
Mchezaji huyo ameonekana kumvisha jezi familia yake na mbwa wake Atom na Humber huku nyuma zikiwa zimeandikwa jina lake. Atom (kushoto) na Humber (kulia) wakipelekwa ndani ya Lowry Hotel ambapo Sanchez ndipo alipofikia Mama mzazi wa Sanchez akiungana na mwanae Lowry Hotel.