DKT. MWAKYEMBE ATOA SALAMU ZA POLE KIFO CHA JUMANNE NTAMBI

http://ift.tt/2nbACsX

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amepokea kwa majonzi taarifa ya kifo cha Kocha Msaidizi wa timu ya Mwadui FC Ndg. Jumanne Ntambi Kilichotokea usiku wa tarehe 23 Januari, 2018 mkoani Shinyanga.
TAARIFA KWA UMMA

Dkt. Mwakyembe amesema kifo chake kimeacha pengo kubwa siyo tu kwa klabu ya Mwadui bali kwa sekta ya michezo ambayo marehemu aliitendea haki kutokana na umahiri wake katika kufundisha soka.

Dkt. Mwakyembe ametoa pole kwa familia ya marehemu, Uongozi wa Klabu ya Mwadui, Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Nchini (TAFCA), Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Wachezaji na Mashabiki wa Klabu ya Mwadui, ndugu, jamaa, marafiki na wanamichezo wote nchini na kuwaombea Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Wakati wa uhai wake marehemu Ndg. Ntambi alifundisha vilabu vya Kahama United ya Shinyanga, Mlale JKT ya Ruvuma, Panone ya Kilimanjaro, Timu ya Mkoa wa Shinyanga na Igembe Nsabo. Hadi anafikwa na umauti marehemu Ntambi alikuwa akiifundisha timu ya Mwadui FC ya Shinyanga akiwa kama kocha msaidizi.

Popular posts from this blog