BREAKING NEWS: AUBAMEYANG ATUA ARSENAL KUONGEZA NGUVU

http://ift.tt/2Eqyp4M

Mshambuliaji mpya wa timu ya Arsenal Pierre Aubameyang (28). VURUGU za usajili barani Ulaya zimeendelea kushika kasi huku Arsenal leo wamemtambulisha staa wao mpya Pierre Aubameyang (28) leo mchana atakuwa akilipwa paundi £180,000 kwa wiki.

Hata hivyo, staa huyo aliyetoka timu ya Borrusia Dortmund amekuwa akionyesha kiwango cha hali ya juu sana kwa misimu ya hivi karibuni. Arsenal wanaonekana kulamba dume pamoja na kwamba wamemuachia mshambuliaji wao Alexies Sanchez ambaye amekwenda kujiunga na Manchester United.

wamemsajili mshambuliaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 55, akiwa ndiye mchezaji aliyesajiliwa ghali zaidi kwenye timu hiyo ya London.

Awali Arsenal walitaka kumpeleka Giroud kwenye kikosi cha Dortmund kwa ajili ya kukamilisha dili la Aubameyang lakini mchezaji huyo mwenye thamani ya pauni milioni 35, aligoma kwenda Ujerumani na kusema kuwa familia yake inataka kubaki London.

Popular posts from this blog