AZAM FC YAITANDIKA SHUPAVU 5 KOMBE LA SHIRIKISHO

http://ift.tt/2DIyJuz

Ikiwa ni siku chache baada ya kupoteza mechi yake ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga, Azam FC imeibukia katika michuano ya Kombe la Shirikisho na kutoa adhabu kali. Timu hiyo, ilivana na Shupavu inayoshiriki Ligi Daraja la Pili katika mchezo huo uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Katika mechi hiyo shujaa wa mchezo huo ni kinda, Paul Peter wa Azam ambaye alipiga ‘hat trick’ katika mechi hiyo katika ushindi wa mabao 5-0. Katika mchezo huo Azam ilionekana kumiliki mpira vyema katika vipindi vyote viwili huku bao la kwanza kwenye mchezo huo likifungwa dk 45 ya mchezo huku la pili likafungwa dakika hiyohiyo baada ya kuongezwa dakika mbili. P

eter alifunga mabao katika kipindi cha pili cha mchezo huo akifunga dakika ya 57, 77 na 88 huku timu yake ikitangulia katika hatua hiyo ya 16 bora. Mabao mengi ya timu hiyo yalifungwa na Yahya Zaydi katika dakika ya 45 kwa njia ya penalti kabla ya Iddi Kipagulile kumchabua kipa wa Shupavu katika dakika za nyingeza baada ya kuwatoka mabeki wa timu hiyo.

Popular posts from this blog