MANCHESTER UNITED WAITANDIKA BENFICA,CHELSEA CHALI,PSG YAUA

http://ift.tt/2iRgxtg

Jana usiku kulikuwa na michezo nane katika viwanja tofauti tofauti barani Ulaya kwenye michuano ya Klabu bingwa barani humo ambapo klabu kubwa zimeendeleza ubabe kwenye michuano hiyo kwa ushindi mnono huku klabu ya Chelsea ikikubali kichapo cha goli 3-0 kutoka kwa klabu ya Roma ya Italia.

Kwenye mchezo wa Roma dhidi ya Chelsea, Chelsea walionekana kuelemewa tangu kipindi cha kwanza na kuruhusu magoli mawili kutoka kwa mshambuliaji wa Roma, Stephan El Shaarawy kabla ya goli la tatu kipindi cha pili.

Nayo klabu ya PSG ya Ufaransa iliendeleza ubabe kwa kuichakaza Anderlecht goli 5-0. Magoli ya Veratti, Neymar na Hat-Trick kutoka kwa Layvin Kurzawa zilikamilisha salio la goli 5-0.

Man United nao wakiwa nyumbani Old Trafford wamepata ushindi mnono wa goli 2-0 dhidi ya klabu ya Benfica.

Bayern Munich nao wamepata ushindi mwembamba wa goli 2-1 ugenini dhidi ya klabu ya Celtic.

Matokeo mengine Barcelona wamelazimishwa sare tasa ya bila kufungana na klabu ya Olympiacos.Tazama matokeo mengine

Popular posts from this blog