Madrid hoi Ujerumani, City na PSG sare
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema bado wana matumaini |
Ligi ya mabingwa barani ulaya imeendelea kwa michezo miwili ya robo fainali kuchezwa.
Wolfsburg wakiutumia vyema uwanja wao wa Volkswagen Arena, wamepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Real Madrid.
Ricardo Rodriguez ndiye alianza kuipatia timu yake bao la kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya Andre Schurrle kufanyiwa madhambi na Casemiro.
Katika dakika ya 18 Max Arnold akaongeza bao la pili na kuwazamisha kabisa vijana wa Zidane.
Nao Man City wakicheza ugenini huko nchini Ufaransa walikwenda sare ya kufunga kwa mabao 2-2, mabao ya Psg yalifungwa na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic na Adrien Rabiot.
Huku mabao ya Man City yakifungwa na viungo Kevin De Bruyne na Fernandinho, mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic alikosa mkwaju wa penati uliokolewa na kipa Joe Hart.